Klabu ya soka ya Everton imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa ligi kuu ya England.
lukaku akiwa anashangilia goli alilofungia timu yake
afunga goli la pili kwenye klabu ya everton
West Brom ndio walianza kupata mabao yao mapema kupitia kwa mshambuliaji Saido Berahino, bao lililofugwa dakika ya 41 ya mchezo,huku Craig Dawson, akiongeza bao la pili dakika 54.
Dakika moja baada ya West Brom kupata bao la pili mshambuliaji machachari wa Everton Romelu Lukaku, akafunga bao la kwanza kisha Haruna Kone, akaongeza bao la pili dakika ya 75.
Zikiwa zimesalia dakika sita mchezo kumalizika Romelu Lukaku, tena akatupia kambani bao la tatu la ushindi.
Everton ilimiliki mchezo kwa asilimia 54 huko wenyeji wa mchezo huo West Brom wakimiliki kwa asilimia 46, mchezo uliochezeshwa na mwamuzi Robert Madley.
No comments:
Post a Comment