Saturday, 24 March 2018

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah



Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri,, huku mechi hiyo ikiisha kwa Ureno kuondoka na ushindi wa 2-1

Mohamed Salah alianza kwa kufunga goli la kwanza kwa mchezo huo ndani ya dakika 56, na kuifanya Misri iongoze kwa muda wote wa mchezo.

Katika sekunde 120 za mwisho wa mchezo Ronaldo alifunga magoli mawili ya kichwa na kuipa timu yake ushindi.

Mechi nyingne kali ni pamoja na mabingwa wa dunia Ujerumani walipolazimishwa  sare na Hispania na kuifanya mechi hiyo iishe kwa sare ya 1-1

Rodrigo na Muller ndo wafungaji wa magoli katika mechi hiyo.

Jesse Lingard amefunga goli lake la kwanza kwa timu yake ya taifa na ni goli la pekee katika mechi hiyo huku Uingereza wakiondoka na ushindi dhidi ya Uholanzi.


Matokeo ya mechi nyingine ni 
Argentina 2   -  0  Italia 
Ufaransa  2   -   3 Colombia 
Urusi        0    -   3 Brazili 
Japani      1   -    1 Mali

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...