Saturday, 2 December 2017

makundi ya kombe la dunia haya hapa..

Droo ya Kombe la Dunia 2018 imefanyika jana jioni ambapo Ureno na Hispania zimepangwa pamoja katika Kundi B.

Hiyo inamaansha Cristiano Ronaldo wa Ureno atacheza dhidi ya Hispania nchi anakochezea katika timu ya Real Madrid. 

Katika droo hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Serikali wa Kremlin Palace, miongoni mwa walioudhuria ni Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino.

Michuano hiyo ambayo ni mikubwa katika ngazi ya soka kuliko yote duniani inatarajiwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 15, ambapo nchi 32 zitashiriki kutoka mabara matano.

Kutakuwa na viwanja 12 na miji 11 ambayo itatumika katika michuano hiyo.

Makundi yalivyopangwa haya hapa.
Kundi A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay
Kundi B: Ureno, Hispania, Morocco, Iran
Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark
Kundi D: Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria
Kundi E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden, Korea Kusini
Kundi G: Ubelgiji, Panama, Tunisia, England
Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...