Ben carson amezaliwa tarehe 18/09/1951 ni jina lenye
mvuto na kutamkika na watu wengi zaidi duni ani kwa sasa
Dr. ben carson kwa sasa
ametajwa kushiriki katika kinyang’anyiro cha kugombea uraisi wa marekani ila
mwana harakati huyu alisema maneno ambayo watu wa dhehebu lingine wameshindwa
kumuelewa
Mgombea huyu wa chama cha
republican amesema hatomsapoti mgombea yeyote ambaye ana dini ya kiislamu
Amesema muislamu hafai
kuwa raisi wa marekani kwasabau tu wanakinzana na katiba ya marekani
Ben Carson, ambaye ni, daktari wa
neva aliyestaafu, amesema yeye katu hawezi kukubali Mwislamu kuwa rais wa
Marekani.
Akijibu maswali katika kipindi cha mahojiano cha runinga ya NBC
''Meet the Press, Carson anasema kuwa dini hiyo inakinzana na katiba ya Marekani.
Kura ya maoni inaonesha kuwa daktari huyo ambaye ni mkristo
anashikilia nafasi ya pili kwa umaarufu nyuma ya bilionea mbishi Donald Trump
Matamshi yake yanatokea siku chache, baada ya
mgombea anayepigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican, Donald Trump,
kukataa kujitenga na mfuasi wake, ambaye alimshutumu Rais Obama kuwa Mwislamu,
na hata sio Mmarekani.
Source BBC swahili
No comments:
Post a Comment