Klitschko kuzirusha dhidi ya Fury
Bingwa wa ulimwengu wa uzani wa juu Vladmir Klitschko na bondia Muingereza ambaye hajashindwa pigano lolote Tyson Fury watapanda ulingoni mnamo Oktoba 28 kwa pigano la kuwania taji la ulimwengu la heavyweight.
Klitschko hajawahi kushindwa mchuano wowote kwa miaka 11, lakini Fury ana rekodi ya kushinda michuano yote 24 aliyoshiriki.
Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 26 atasafiri kwenda Ujerumani ili kujaribu kumponya taji bingwa wa dunia Klitschko, ambaye alipigana kwa mara ya mwisho mwaka wa 2010 mjini Dusseldorf. Klitschko ambaye ana mataji ya WBA, WBO, IBF na IBO, amesema ana uhakika Tyson Fury atafanya juu chini kulinyakua taji hilo. "Nadhani utakumbana na pigano gumu kabisa la maisha yako. Nadhani haitakuwa rahisi kwako na naamini pia nitapambana na mmoja wa wapinzani wagumu kabisa. Ukubwa wako, na urefu, mbinu zango ulingoni itakuwa changamoto pia. Lakini ntakuwa tayari. Naahidi".
Tyson Fury ambaye ndiye aliyetangazwa kuwa mpinzani wa lazima wa taji la WBO mwezi Novemba mwaka jana, ana matumaini makubwa na anasema ana hamu ya kupanda ulingoni kwa pambano hilo. "Sina hamu na mataji yote na mikanda yote uliyo nayo. Nina hamu ya kuuvunja uso wako. Hilo ndio ninalotaka. Unachosha. Ninataka kuondoa katika kitengo cha uzani wa heavyweight. Ulaya yote inataka kuona ukipigwa. Na Ulaya yote na ulimwengu mzima utaona ukizabwa".
No comments:
Post a Comment