Tuwe pamoja kwenye mada hii kujuzana kile kinachojiri mechi ya The Flames Vs Taifa Stars kutoka uwanja wa Kamuzu. Taifa Stars imeshawasili mjini wa Blantire kwa basi kutoka Lilongwe ambako walitua. Kuingia uwanja wa Kamuzu inahitaji kuwa na angalau Kwacha 1000 sawa na Tshs 4000 kwa hela za nyumbani, mechi itarusha na Supersport 9 na wanaotumia king'amuzi cha Azam wanaweza kuona kupitia Malawi TV. kuanzia saa tisa kamili alasiri.
Kocha Mkwasa akiongea mapema kidogo amesema timu haina majeruhi na amesema kutakuwa na game plan tofauti kidogo na Nazir naye kasema leo watajitahidi kutoruhusu goli ili wajihakikishie kusonga mbele.
Kikosi cha stars leo kitakuwa na wachezaji wake mahiri.
- Ally Mustapha
- Shomari Kapombe
- Haji Mwinyi
- Kelvin Yondani
- Nadir Haroub
- Himid Mao
- Thomas Ulimwengu
- Mudathir Yahya
- Mbwana Samata
- Said Ndemla
- Farid Mussa
00' Filimbi imeshapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo huu
35' Taifa stars wanakosa goli baada ya kufanikiwa kupata kona
42' Gooool, Malawi wanafunga bao la kwanza baada ya John Banda kutia nyavuni 1-044' Mudathir anapewa kadi ya njano na faulo inapigwa kelekea Malawi na Shomari Kapombe lakini haikuzaa matunda.
45+1' Mpira sasa ni mapumziko na matokeo yanasimama Malawi 1-0 Tanzania
46' Mpira umerejea baada ya mapumziko
60' Malawi wanafanya badiliko la wachezeji
70' Yondani anaondoa hatari langoni mwa Taifa Stars
72' Ulimwengu anawekwa chini na faulo kuelekea Malawi, Himid Mao anapiga lakini unatoka nje
73' Mustapha Bartez anaondoa mpira baada ya lango la taifa stars kuwa katika hatari
74' Mbwana Samatta anafika langoni mwa Malawi lakini mpira unatoka nje
76' Kuna sintofahamu na John Boko na Mzava wa Malawi wote wanapewa kadi za njano, mpira unaelekea Taifa stars
78' Mrisho Ngassa anaingia kuchukua nafasi ya Farid Mussa pia Malawi wanafanya mabadiliko
90' Malawi wanapata kona lakini haikuzaa matunda'
90' Zinaongezwa dakika nne
90+3' Samatta anapewa kadi ya njano baada ya kupanda na kushuka kwenye machela
90+4' Ulimwengu anabebwa kwenda nje
90+5' Pyeeee, kipenga kuashiria mwisho wa mchezo
Matokeo yanaisha kwa Stars kufungwa goli moja lakini wanasonga mbele baada ya kuongoza matokeo ya jumla kwa 2-1. Timu inarejea kesho na baada ya ushindi huu itakutana na Algeria.
ANGALIA GOLI WALIVYOPATA MALAWI
https://youtu.be/4Rb3slhnjhU
SOURCE JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment