Sunday, 11 October 2015

WASIFU WA EDWARD NYONYAI LOWASA MGOMBEA URAISI WA CHADEMA

WASIFU WA EDWARD LOWASA
GENERAL

SalutationHon.Member picture
First Name:Edward
Middle Name:Ngoyai
Last Name:Lowassa
Member Type:Elected Member
Constituent:Monduli
Political Party:Chama Cha Mapinduzi
Office Location:P.O. Box 139, Monduli
Office Phone:+255 754 800000Office Fax:+255 22 2452037
Office E-mail:elowassa@parliament.go.tz
Member Status:Active
Date of Birth26 August 1953
EDUCATION
School Name/LocationCourse/Degree/AwardStart DateEnd DateLevel
Monduli Primary SchoolCPEE19611967Primary School
Arusha Secondary SchoolCSEE19681971Secondary School
Milambo Secondary SchoolACSEE19721973Secondary School
University of Dar Es SalaamBA (Edu) Hons.19741977Bachelor
University of Bath, UKMSc. (Development Studies)19831984Masters Degree
EMPLOYMENT HISTORY
Company NamePositionFromTo
Tanzania GovernmentPrime Minister20052/8/2008
Ministry of Water and Livestock DevelopmentMinister20002005
State, Vice President's OfficeMinister for Environment & Poverty19972000
The Parliament of TanzaniaMember - Monduli Constituency19952015
Ministry of Lands, Human Settlement DevelopmentMinister19931995
State, Prime Minister's Office and First Vice PresidentMinister (Judiciary &Parliamentary Affairs)19901993
Arusha International Conference CentreManaging Director19891990
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
Chama Cha Mapinduzi, CCMMember1990Todate
Chama Cha Mapinduzi, CCMParty Executive-District, Regional &Head Office19771989
Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Mshika bendera wa muungano wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao ambaye pia alikuwa ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa .
Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama.
Kabla ya kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka 1977.
Hatua ya mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Tanzania kuamua kujiunga na chama cha upinzani Chadema, ikiwa imebaki miezi mitatu tu kuelekea uchaguzi mkuu, imebadilisha kabisa upepo wa kisiasa nchini Tanzania, na hasa uchaguzi mkuu ujao.


Image captionWasifu wa Lowassa

Lowassa alikuwa Maziri Mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008 kabla ya kujiuzulu wadhifa huo kufuatia kashfa ya rushwa iliyohusisha kampuni ya kuzalisha umeme ya ki-Marekani Richmond Development Company LLC ya Houston Texas.
Hata hivyo wakati anatangaza kuhamia kwake Chadema, Lowassa alikanusha katu kuhusika kwa namna yoyote na kashfa hiyo na kudai kuwa yeye alifuata tu amri kutoka kwa ‘wakubwa’ walio juu yake.
“Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa


Image caption“Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa

Kuhama kwake kunamfanya Lowassa kuwa ndie kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu kabisa wa CCM kukihama chama hicho tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mnamo mwaka 1992.
Mwanajeshi wa zamani na aliyewahi kupigana wakati wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka 1978/79, Lowassa aliiambia hadhara kwamba akiwa kama mtu mwenye uchungu na nchi yake isingekuwa rahisi kubaki ndani ya CCM huku akiona chama hicho kimepoteza mwelekeo na sifa ya kuongoza nchi.
Lowassa alikimbilia upinzani baada jina lake kukatwa wakati alipoomba kuwa mgombea urais kupitia chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika baadaye mwezi huu .
Wakati mchakato wa CCM wa kumtafuta mgombea wao wa urais ulipoanza, Lowassa ndiye aliyekuwa kinara wa wagombea wote 42.
Kila kona aliyozunguka, mikutano yake ya hadhara ilivutia maelfu ya watu waliomuunga mkono.
Wakati chama cha CCM kilimtaka kila mgombea apate sahihi za wadhamini 450 lakini Lowassa alipata sahihi za wadhamini zaidi ya 700,000.


Image captionWasifu wa Edward Lowassa

Hata hivyo mchujo wa chama ulipofanyika jina lake lilikatwa mapema kabla hata ya kupelekwa kwenye vikao vya vya juu vya chama hicho. Ambapo baadae Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka kidedea na kuwa mgombea kupitia chama tawala CCM.
Lowassa ameushutumu mchakato CCM wa kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na mizengwe dhidi yake, hali ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa demokrasia’
“Nitakuwa mnafiki nikisema bado nina imani na CCM.''
''CCM niliyoiona Dodoma si CCM niliyokulia”, alisema, na kuongeza “kama Watanzania hawapati maendeleo kupitia CCM basi wakayatafute nje ya CCM”
Wakati sakata la Richmond lilipoibuka miaka michache tu iliyopita, Chadema ilimfanya limsakame Lowassa kuwa ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini.
Lakini wakati chama hicho kinamkaribisha kuwa mwanachama wao, kiligeuka na kusema hakuna mtu msafi nchini na kwamba hawawezi kuacha kumpokea mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa wafuasi kama Lowassa.
Wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa moja wa shughuli za serikali.
Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la ‘Mzee wa maamuzi magumu’.
Moja ya mafanikio makubwa ya uwaziri mkuu wake ni jitihada kubwa na mafanikio ya upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma.


Image captionJe unamfahamu Edward Lowassa ni nani katika siasa za Tanzania ?

Chuo hiki kikuu cha umma kilichopo katikati ya Tanzania kilianzishwa mwaka 2007.
Lowassa ni mashuhuri pia kwa kusimamia mpango wa serikali uliofanikiwa wa ujenzi wa shule za kata ambazo uliiletea Tanzania sifa kubwa kwa kutoa fursa ya watoto wengi kupata nafasi shuleni.
Mtoto wa Mzee Ngoyai Lowassa, ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni, Lowassa ameanza harakati zake za kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini inaarifiwa kwamba rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alimkatalia kushika nafasi hiyo.
Wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo
Ulipofika uchaguzi wa mwaka 2005, Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala yake alimnadi rafiki yake wa siku nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...