Toyota imekuwa kampuni ya magari ya hivi karibuni kujaribu gari linalojiendesha bila dereva katika barabara ya uma.
Gari hilo aina ya Lexus GS lilijaribiwa katika barabara ya Tokyo Shuto Express ambapo lilionyesha ubora wake, ikiwemo kubadilisha laini za barabara na kukaa mbali na magari mingine.
Toyota imesema kuwa inalenga kuanzisha magari kama hayo ifikiapo mwaka 2020,wakati ambapo mji wa Tokyo utakuwa ukijiandaa kusimamia mashindano ya Olimpiki.
Kulingana na Toyota, gari hilo linatumia sensa kadhaa ili kubaini magari yalio karibu na kuchagua laini za barabara kwa lengo la kufika linakoelekea.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa gari hilo linaendesha usukani, kichapuzi na breki sawa na vile binadamu wanavyoendesha magari yao.
Kampuni hiyo inasema kuwa inapanga kuzindua gari hilo katika soko mwaka 2020, lakini haijasema iwapo itatengeza magari yatakayojiendesha katika barabara za mitaani.
http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151009_toyota-driverless
No comments:
Post a Comment