Monday, 21 March 2016

REA:KIKAO CHA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, PROF. SOSPETER MUHONGO NA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI AWAMU YA PILI - TAREHE 29 HADI 31 MACHI, 2016

Monday, March 21, 2016|

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (MB) ameandaa kikao cha siku tatu kwa ajili ya kukutana na wakandarasi wakubwa (Main Contractors) na wakandarasi wadogo (Sub-Contractors) wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini Awamu ya Pili kwa lengo la kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Vikao hivyo vitafanyika kuanzia tarehe 29 hadi 31 Machi, 2016 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini. Kila mkandarasi azingatie muda uliooneshwa kwenye ratiba na barua walizotumiwa.


Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)
20 SAM NUJOMA, 14414
P. O. BOX 7990
DAR-ES-SALAAM.
source: http://rea.go.tz/NewsCenter/Announcements/tabid/139/Default.aspx 

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...