Monday, 21 March 2016

MATOKEO YA URAISI ZANZIBAR, SHEIN ASHINDA KWA KISHINDO


MATOKEO RASMI:
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha amemtangaza Dr. Mohammed Shein kuwa Rais wa Zanzibar kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016 kwa asilimia 91.4.
shein.jpg 
Dr. Mohammed Shein

Kwa mujibu wa Jecha, Shein amepata ushindi wa kishindo wa kura 299,982 ambazo ni sawa na asilimia 91.4. Nafasi ya pili imeshikiliwa na mgombea urais wa ADC, Hamad Rashid aliyepata kura 9,734 huku Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 6,076.

Kutokana na matokeo hayo, Dk. Ali Mohamed Shein ndiye atakayeendelea kuiongoza Zanzibar kwa muhula wake wa mwisho kwa mujibu wa Katiba.
matokeo.jpg

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...