Wednesday, 24 August 2016

kenya waongoza medali kutoka RIO olympic 2016

Rio Olympics Athletics
Eliud Kipchoge wa Kenya akimaliza marathon Rio de Janeiro, Brazil, Aug 21, 2016.
Mkenya Eliud Kipchoge ameipatia Kenya medali nyingine ya dhahabu baada ya kushinda mbio za marathon katika muda wa saa 2, dakika 8.44 mjini Rio de Janeiro Jumapili.
Kipchoge aliongoza mbio hizo kwa karibu nusu nzima ya mwisho ya shindano hilo huku akipambana vikali na Feyisa Lilesa wa Ethiopia na Galen Rupp wa Marekani ambao baadaye walimaliza wa pili na wa tatu.
Mtanzania Alphonse Felix Simbu alimaliza katika nafasi ya tano ikiwa ni nafasi ya juu kabisa kwa Mtanzania katika mbio za marathon katika kipindi kirefu.
Solomon Mutai wa Uganda alimaliza katika nafasi ya nane, na kufanya wanartiadha wa Afrika Mashariki kushika nafasi nane za kwanza katika mbio hizo.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...