Kocha huyo wa Manchester United amemsifia Eric Bailly baada ya kuibuka nyota wa mchezo katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City
Mourinho alifurahishwa na jinsi Bailly alivyoweza kukabiliana vema na washambulizi wa Leicester City katika dimba la Wembley na pia alimpa sifa beki mwenzake Daley Blind kwa ushirikiano mwema na mwenzake.
"Nadhani Bailly alikuwa mpinzani wao sahihi kwa sababu ana kasi kama walivyokuwa washambulizi wao. Namfahamu ni aina gani ya mchezaji, lakini mara zote alama ya kiulizo huibuka mchezaji anapoonesha kiwango kikubwa kuliko kile kilichotarajiwa," Mourinho alikiambia BT Sport.
"Lakini kuja Manchester United na kucheza mechi yako ya kwanza rasmi katika uwanja wa Wembley na majukumu kama haya, bila ya [Chris] Smalling - alifanya vema mno. Lakini pia sina budi kusema kwamba Daley Blind alimsaidia kumpa msaada aliohitaji kwa sababu naye katika kipengele cha ulinzi yuko vizuri."
Nyota mwingine wa United aliyesajiliwa majira ya joto, Zlatan Ibrahimovic alifunga goli la ushindi kuipa Manchester United mwanzo mzuri katika ufunguzi wa pazia la msimu mpya
No comments:
Post a Comment