Friday, 12 August 2016

Viongozi wa Republikan wanaomkataa Trump waongezeka

Trump Banner
nafasi ya kushinda urais kwa trump inazidi kufifia kila kukicha

Kwa mara ya pili wiki hii, kundi la Warepublikan mashuhuri hapa Marekani, linasema kuwa halitamuunga mkono mgombea wa urais wa chama hicho, Donald Trump. Zaidi ya wanchama 70, wakiwa ni pamoja na wabunge wa zamani na wanachama waandamizi wakati wa utawala wa marais Ronald Reagan, George Walker Bush na George Bush, wameandika rasimu ya barua kwa mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya chama hicho, RNC, REINCE PRIEBUS.
Wanaitaka RNC kuacha kutumia pesa za chama, wakati, na wafanyakazi wake na kulipia matangazo ya kumuunga mkono Donald Trump. Badala yake, wanataka fedha hizo kutumika katika kampeni za wagombea wa viti vya bunge na senate, wa chama hicho. Wanasema kuwa uwezekano wa Trump kushinda mwezi Novemba unaendelea kufifia kila siku.
Miongoni mwa sababu wanazotoa wanachama hao, ni malumbano ya Trump na wazazi wa mwanajeshi Mmarekani Muislamu aliyeuawa akiwa vitani Iraq, matamshi yake kwa waunga mkono haki ya kumiliki bunduki kumshughulikia mpinzani wake wa chanma cha Demokratik Hillary Clinton, na ‘kusema kila aina ya uwongo kuhusu maswala madogo na makubwa. Kufikia Ijumaaa asubuhi, kampeni ya Trump haikuwa imelizungumzia swala hilo.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...