Kura zimeanza kuhesabiwa huko Zambia baada ya uchaguzi mkuu wa rais na bunge kufanyika jana kwa Amani, kukiwepo na idadi kubwa ya wapiga kura walojitokeza , kufuatia kampeni zilizokumbwa na ghasia. Tume ya uchaguzi imetangza kwamba matokeo yataweza kutangazwa pole pole na matokeo ya mwisho rasmi yanatarajiwa siku ya jumamosi.
Wachambuzi wanasema ni vigumu kujua nani ataashinda kati ya rais Edgar Lungu anaetetea nafasi yake au kiongozi wa upinzani HAKAINDE HICHILEMA.
Alhamisi jioni Polisi wa Zambia, walikanusha vikali ripoti za vyombo vya habari kwamba baadhi ya raia wa kigeni wamekamatwa kwa sababu ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu huo.
Msemaji wa polisi RAE HAMONGA, aidha aliiambia Sauti ya Amerika kuwa ujumla, uchaguzi huo ulifanyika kwa amani, licha ya visa vichache vya vurugu za hapa na pale. Polisi walikuwa na jukumu muhimu la kuhakikisha kuwa zoezi hilo lilikuwa la amani, ikiwa ni pamoja na kulinda vifaa vilivyotumika katika uchaguzi mkuu na ule wa kura ya maoni.
No comments:
Post a Comment