Thursday, 8 September 2016

Korea Kaskazini yapuuza shutuma za Baraza la Usalama la UN

 Korea Kaskazini yapuuza shutuma za Baraza la Usalama la UN

Korea Kaskazini yapuuza shutuma za Baraza la Usalama la UN

Korea Kaskazini imepuuza shutuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufutia makombora matatu yaliyorushwa na nchi hiyo Jumatatu ya juma hili. Korea Kaskazini imesisitiza kuwa itaendelea na mipango yake ya nyuklia na makombora.

Juzi Jumanne, nchi hiyo ilishutumiwa katika tamko la baraza hilo lililokosoa vitendo vyake vya kurejelea kurusha makombora hayo. Makombora hayo yanaaminika kuanguka kwenye ukanda wa kiuchumi wa Japani uliopo kwenye Bahari ya Japani.

Shirika la habari linaloendeshwa na Korea Kaskazini ilitoa taarifa iliyosomwa na msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo jana Jumatano. Ilisema kuwa shutuma hizo ni uingiliaji usiokubalika wa uhuru wa nchi hiyo kujilinda na kuongeza kuwa Korea Kaskazini haikubaliani kabisa na tamko hilo.
SOURCE: NHK

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...