Tuesday, 28 February 2017

Bossou avurugana na mashabiki wa klabu yake



Hali inaonekana kuwa si shwari kihivyo ndani ya klabu ya Yanga, hasa baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumshambulia beki Vincent Bossou mtandaoni.


Mashabiki wa Yanga wanaonyesha kuchukizwa na Bossou kutokana na uamuzi wake wa kutotaka kucheza katika kikosi hicho.



Taarifa zinaeleza Bossou amegoma kucheza kwa kuwa anadai mshahara wake wa miezi kadhaa.


Lakini kupitia mtandao wa Instagram, Bossou amesema anaidai Yanga mshahara wa miezi minne.


Ingawa Bossou Kingereza chake ni cha "kuunga" amewajibu mashabiki wa Yanga, kwamba yuko tayari kuondoka ila wamlipe mshahara wake wa miezi minne.


Beki huyo raia wa Togo, tayari ametishia kuondoka Yanga, hali inayoonyesha mambo hayajakaa vizuri kwa kuwa mshambuliaji Donald Ngoma naye amekuwa akielezwa kuwa mgonjwa lakini kuna taarifa kuwa anafanya mgomo baridi.
source: Salehe jembe

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...