Mechi
wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga uliochezwa wikiendi iliyopita
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ulikusanya kiasi cha fedha cha shilingi
milioni 324.
Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema
mapato hayo yamepatikana baada ya kupiga hesabu za mashabiki
waliojitokeza kutazama pambano hilo.
“Mechi
ya Simba na Yanga imeingiza kiasi cha shilingi milioni mia tatu
ishirini na nne laki moja na themanini, hiyo ni baada ya mashabiki wa
pande zote kujitokeza kuliangalia pambano hilo ambalo lilikuwa na
ushindani wa aina yake.
“Kwenye
fedha hizo, Simba watapata asilimia 40 (Sh milioni 129.6) ya fedha zote
kwa sababu ya uenyeji wao, Yanga wakichukua asilimia 20 (Sh milioni
64.8) ya mapato yote kwa sababu wao walikuwa wageni wa pambano hilo.
“Lakini
pia kuna taasisi ambazo zitachukua sehemu ya mapato hayo ambayo ni TFF
asilimia 5, VAT asilimia 18, Selcom wao asilimia 5, Baraza la Michezo
Taifa (BMT) asilimia 1 na Chama Cha Soka Dar es Salaam (DRFA) asilimia
3.
“Nyingine
ni gharama ya uwanja asilimia 15, Bodi ya Ligi (TPLB) wao asilimia 9,
gharama ya mchezo mzima ulivyokuwa ikihusisha maandalizi asilimia 7,”
alisema Lucas.
No comments:
Post a Comment