Monday, 22 May 2017

Juventus bingwa wa ligi ya Seria A kwa msimu wa sita mfululizo

Juventus players celebrate with coaches and club officials with the famous trophy centredVibibi vizee vya Turin Klabu ya Juventus imeweka historia ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya nchini Italia kwa mara ya sita mfululizo .
Juventus wametwaa ubingwa huo wa Seria A baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya vibonde wa ligi hiyo klabu ya Crotone.
Mabao ya ushindi ya Juve katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji Mario Mandzukic katika dakika ya 12 ya mchezo , Paulo Dybala akaongeza bao la pili katika dakika ya 39, Mlinzi Alex Sandro akapiga msumari wa mwisho katika dakika ya 83.
Hili ni kombe la pili kwa timu hiyo baada ya wiki iliyopita kutwaa taji la Copa italia kwa kuichapa Lazio kwa mabao 2 -0.
Massimiliano Allegri is covered with referee's 'invisible spray' by forward Juan Cuadrado
kocha wa klabu ya juventus akimwagiwa unga wa mwamuzi baada ya kushinda kombe la ligi kuu italia
Allegri, winning his third Serie A title as Juventus manager, celebrates with his wife and child
allegri akiwa na mke wake pamoja na mtoto wake wakiwa na furaha baada ya kuchukua kombe

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...