Monday, 22 May 2017

harry Kane mfungaji bora wa ligi kuu uingereza

KaneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMfungaji bora wa ligi ya England kwa msimu wa pili mfulizo Harry Kane
Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Kane ameibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa msimu wa 2016/2017.
Mshambuliaji huyo amemaliza msimu kwa kufunga jumla ya mabao 29 akiwa kacheza kwa dakika 2531, huku akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 87.
Kane anaibuka mfungaji bora kwa msimu wa pili mfululizo msimu uliopita alifunga mabao 25 na kuwa mfungaji bora.
Haki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionRomelu Lukaku amemaliza msimu na mabao 25 goli nne nyumba ya Harry Kane
Wachezaji wanaofuati kwa ufungaji bora ni Romelu Lukaku wa Everton mwenye magoli 25 akifuatiwa na Alexis Sánchez wa Arsenal mwenye mabao 24.
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amemaliza msimu akiwa na magoli 20, nae Sergio Aguero akimaliza na mabao 20.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...