Shabiki maarufu wa Yanga, Ally Yanga amekutana na kipigo kikali kutoka kwa mashabiki walioelezwa ni wa Simba wanaoiunga mkono Mbao FC.
Mashabiki hao wa Mwanza, wamempiga Ally Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kabla ya Yanga kuivaa Mbao FC kwenye uwanja huo, leo.
Yanga inaivaa Mbao FC kuwania kucheza fainali dhidi ya Simba ambao jana wameufunga Azam FC kwa bao 1-0 na kutinga fainali.
Mmoja wa mashabiki wa Simba mjini Mwanza, Fred Bundala ameiambia SALEHJEMBE, Ally Yanga alilazimisha kuingia uwanjani na kumwaga vitu ambavyo wao waliamini ni ushirikina.
“Mwanzo tulimueleza kistaarabu, hakusikia. Tukamsisitiza, akaanza kutoa maneno ya kashfa, nyie watu wa Dar mna dharau sana. Tukaona acha tumkaribishe Mwanza,” alisema.
Ally Yanga alionekana akiwa anatema mate yenye damu baada ya kushambuliwa na mashabiki hao ambao walionekana wengi kuliko wa Yanga.
Juzi, mashabiki wa Yanga walikesha uwanjani hapo wakiulinda uwanja huo kuhakikisha hakuna vitendo vya kishirikina.
Lakini mashabiki wa Mbao FC walilaumu kuwa Yanga wamekuwa wakifanya ushirikina, nao wakaongeza nguvu kuongeza ulinzi usiku wa kuamkia leo.
No comments:
Post a Comment