Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lina mpango wa kupunguza muda wa mchezo wa mpira wa miguu, kuwa dakika 30 kila kipindi.
Bodi ya kimataifa ya soka duniani inatarajia kujadili pendekezo hilo linalolenga kuondoa upotezaji muda kwa makusudi, tabia inayofanywa wachezaji uwanjani.
Aidha waliopendekeza mpango huo wanasema kuwa mechi huchezwa kwa dakika 60 pekee kati ya 90 na muda uliosalia hutumiwa vibaya na wachezaji.
Pendekezo jingine ni wachezaji kutoruhusiwa kupiga mpira mara ya pili baada ya kipa kuupangua wakati wa penalti na iwapo penalti haikupigwa inavyostahili, mchezo utasitishwa na mpira wa adhabu kutolewa.
Mapendekezo mengine ni kama kuweka saa katika uwanja ambayo italingana na ile ya refa mbali pamoja na sheria mpya itakayoruhusu mchezaji kujipigia mpira au hata kutamba na mpira wakati anapopiga mpira wa adhabu
No comments:
Post a Comment