Monday, 19 June 2017

roma mkatoliki afunguka nini kinachomsumbua

Rapa Roma Mkatoliki aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na tungo zake zenye kugusa jamii na maisha ya kila siku ya watu, amefunguka na kusema toka ametekwa na kuachiwa afya yake kiujumla imeimarika ila bado anatatizo katika kidole chake cha mwisho 
Rapa Roma Mkatoliki.
Roma Mkatoliki anadai kuwa kidole hicho kilivunjika lakini hata baada ya kufanyiwa matibabu bado kidole hakijaweza kukaa sawa kwani kimekuwa hakina mawasiliano lakini hakiwezi kumzuia yeye kuendelea na michakato mingine akiamini kuwa ipo siku atapata wataalam ambao wataweza kukinyoosha kidole hicho.
"Unajua niliumia sehemu nyingi ila sehemu ambayo bado haijakaa sawa ni kwenye kidole kwani nilivunjika kwenye kidole cha mwisho tunachokiimba kilivunjika ndiyo maana utaona nilikuwa na muongo muda mrefu zaidi ya wiki sita, tumefungua hongo lakini kama hakijaunga bado hivyo ni kama hakina mawasiliano hakikunji wala hakifanyi chochote, lakini hiki hakinizuia mimi kufanya mambo mengine, Inshalaah kila kinachotokea Mungu huwa na sababu zake labda Mungu hapendi ninyooshe kidole cha mwisho juu tena jukwaani japo siamini katika hilo panapo majaliwa tutapata wataalam wakinyooshe kitakaa sawa" alisema Roma Mkatoliki 
Mbali na hapo Roma Mkatoliki anasema mtandao wake wa Instagram ulikuwa 'hacked' siku mbili baada ya wao kuachiwa huru na mateka hivyo saizi anahangaika kuhakikisha wanairudisha account yake hiyo.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...