Friday, 9 June 2017

leicester City imemteua Craig Shakespeare kuwa kocha wa klabu hiyo

Craig Shakespeare
Leicester City wamemteua kaimu meneja Craig Shakespeare kuwa meneja kamili wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Alikuwa amepewa kazi ya kuwa meneja wa muda Februari baada ya kufutwa kazi kwa Claudio Ranieri.
Shakespeare, 53, ambaye amefanya kazi kama kaimu au mkufunzi msaidizi pekee, alikuwa msaidizi wa Ranieri baada ya kujiunga na klabu hiyo chini ya meneja wa awali Nigel Pearson.
"Hii ni fursa nzuri sana kwangu kuendelea na safari hii mpya katika taaluma yangu," amesema Shakespeare
"Maandalizi yetu kwa mechi za kabla ya msimu na kwa ajili ya Ligi ya Premia yamekuwa yakiendelea kwa muda, lakini sasa tunaweza kuendelea kwa uhakika na kuhakikisha kwamba tuna uwezo wa kutoa ushindani unaotarajiwa kutoka kwa kalbu kama vile Leicester City."
Shakespeare alishinda nane kati ya mechi 16 alizokuwa kwenye usukani Leicester msimu uliopita, na kuongoza pia klabu hiyo kufika robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kama mabingwa watetezi Ligi ya Premia, Leicester walikuwa alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja wakiwa na mechi 13 zilizosalia Ranieri alipoondoka.
Lakini Shakespeare aliwasaidia kushinda alama 23, miongoni mwa hizo akizizoa kwa kushinda mechi zake tano za kwanza na kuwawezesha kumaliza wakiwa nafasi ya 14.
Leicester waliondolewa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Atletico Madrid.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...