Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, hatojiunga na kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuanza mazoezi siku ya Jumanne huku akiendelea kufuatilia uhamisho wake kuondoka Stamford Bridge. (Marca)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa hawatomuuza beki wa kushoto Alex Sandro, 26. (Sport Mediaset)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, baada ya Nemanja Matic kwenda Man Utd. (Mail)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, iwapo Philippe Coutinho, 25, ataondoka kwenda Barcelona. (Bild)
Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, atakuwa na mazungumzo na meneja wake mpya Mauricio Pellegrino, wiki hii, huku Liverpool wakijiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kumchukua beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (Liverpool Echo)
Liverpool wamekataa kukata tamaa katika kumfuatilia beki wa Southampton Virgil van Dijk na watajaribu tena kufanikisha usajili huo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Mail)
Dau la euro milioni 100 kutoka kwa Barcelona kumtaka Philippe Coutinho, 25, limekataliwa na Liverpool. Barca walipanda dau jingine baada ya euro milioni 80 za awali pia kutupiliwa mbali huku Liverpool wakisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi. (RMCSport)
Liverpool wanamnyatia kiungo wa Monaco anayesakwa pia na Arsenal, Thomas Lemar, 21. (Le 10Sport)
Inter Milan wanapanga kutoa dau la pauni milioni 35 kumtaka winga wa Liverpool Sadio Mane. (Daily Express)
Inter Milan huenda wakawazidi kete Arsenal katika kumsajili beki wa Nice, Dalbert, 23, kwa pauni milioni 17. (TMW)
Tottenham na Inter Milan zinafikiria kwanza kabla ya kutaka kumsajili beki wa Paris Saint-Germain Serge Aurier, 24, wakiwa na matumaini kuwa ada yake ya uhamisho itapunguzwa. (La Parisien)
Manchester United wamefikia makubaliano na beki wa kulia Serge Aurier, 24, wa PSG, lakini atalazimika kwanza kwenda mahakamani ili kupewa ruhusa ya kuingia Uingereza. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikutwa na hatia ya kumpiga polisi. (The Mirror)
Newcastle wanamtaka mshambuliaji Lucas Perez, 28, wa Arsenal, lakini hawapo tayari kutoa pauni milioni 13.4 wanazotaka Arsenal. (London Evening Standard)
No comments:
Post a Comment