Tuesday, 12 September 2017

Kotei Mchezaji Bora Mechi ya Simba na Azam

Kotei  Mchezaji Bora Mechi ya Simba na AzamKiungo wa kimataifa raia wa Ghana wa wekundu Msimbazi, James Kotei amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi iliyopigwa jana dhidi ya Azam FC mchezo uliyopigwa katika viunga vya Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Hayo yamewekwa wazi na taarifa iliyotolewa na ukurasa maalum wa Simba SC usiku wa kuamkia leo baada ya timu yao kutoka sare ya bila kufunguna na wapinzani wao wa siku hiyo Azam FC ambapo kila mmoja alitamani kumfunga mwenzake ili aweze kujiwekea rekodi mpya lakini kwa bahati mbaya mambo yakaenda ndivyo sivyo.
"Kiungo mahiri wa Simba, James Kotei amechaguliwa na wapenzi wa Simba kuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Azam FC", imesema taarifa hiyo.

James Kotei amesaini kandarasi ya miaka miwili ya kuwatumikia wekundu wa Msimbazi, Simba SC baada ya kumalizika mkataba wake wa awali aliokuwa akiutumikia hapo msimbazi wa miezi sita

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...