"Kama unanisikia ni miaka 15
sasa imepita, ni imani yetu kuwa upo kwenye makazi mema nasi tunazidi
kukuombea uwe sehemu salama huku tukiamini ipo siku tutaungana na wewe
tena kama familia, baba uliniacha nikiwa mdogo kiasi, lakini nilikuwa na
ndoto kubwa katika maisha yangu mtoto wako nimepitia mambo mengi
makubwa hasa mwaka huu ilifika kipindi niliamini zimesalia dakika chache
niungane na wewe lakini hayakuwa mapenzi ya Mungu, nikaungana na Mama
na tunaendelea na maisha yetu Duniani hapa" aliandika Roma Mkatoliki
Rapa Roma Mkatoliki mwanzoni mwa mwezi April alitekwa na watu
wasiojulikana na kuteswa kiasi cha kuvunjwa mpaka kidole chake cha
mwisho na kisha kujakupatikana siku ya tatu akiwa yeye na wenzake huku
wakiwa na majereha mbalimbali kwenye miili yao. Itazame hapa ngoma yake ya kwanza kutoka baada ya kutekwa ambayo imeweza kujibu maswali kadhaa ambayo watu walikuwa wakijiuliza kipindi alipokuwa ametekwa na yaliyomkuta kwa hao watekaji
No comments:
Post a Comment