Juan Mata alipeana mpira kwa makosa kwa Aaron Mooy katikati ya uwanja na baada ya kumpatia pasi nzuri Tom Ince, ambaye shambulio lake lilipanguliwa na David De Gea, raia huyo wa Australia alikuwa wa kwanza kurejesha mpira huo wavuni kutoka maguu 10 huku safu ya ulinzi ya United ikiangalia.
Baadaye beki wa Sweden Victor Lindelof aliyeingia kama mchezaji wa ziada kuchukua mahala pake Phil Jones aliyepata jeraha alizungukwa na Laurent Depoitre na kuongeza bao la pili kunako dakika ya 33.
Muurinho alifanya mabadiliko katika kipindi cha mapumziko akimuingiza Marcus Rashford na Herikh Mkhitaryan ambapo kijana huyo aliwapatia bao la kufutia machozi ikiwa zimebakia dakika 12 kupitia kichwa kizuri baada ya krosi ya Lukaku.
rashford akifunga goli la pekee kwa manchester united kutoka kwa krosi iliyotoka kwa lukaku
No comments:
Post a Comment