Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema mbio za kuwania ubingwa wa
ligi kuu ya soka nchini England EPL ni kama zimefika mwisho kutokana na
mwendelezo mzuri wa Manchester City.
Akiongea
kuelekea mchezo wa EPL kati ya timu yake ya Liverpool dhidi ya
Tottenham Klopp amekiri hilo kwa kudai haoni nafasi kwa timu zingine
kwasababu Manchester City haioneshi dalili za kukwama.
“Manchester City inafanya vizuri na
nafikiri wananafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa kuliko timu zingine
japokuwa kwenye soka lolote linawezekana amesema”, amesema Klopp
Liverpool ambayo ina pointi 13 katika
nafasi ya 8 imekuwa haina mwendelezo mzuri kwenye ligi japokuwa Klopp
ana imani na timu yake kuwa inaweza kufanya vizuri.
Endapo Liverpool itashinda leo dhidi ya
Tottenham itafikisha alama 18 na kupunguza tofauti ya alama dhidi ya
vinara Manchester City wenye alama 25
No comments:
Post a Comment