Friday, 20 October 2017

Mo dewji awajibu mashabiki wa yanga kuhusu mchezaji wa simba

Mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohammed Dewji ambaye ni shabiki kindakindaki wa Simba amefunguka na kuwaambia wapinzani wao wa jadi Yanga kuwa hawataweza
Mohammed Dewji ameweka picha ya katuni ambayo inamuonyesha mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba Ibrahim Ajib ambaye sasa anakipiga Yanga akifurahia ushindi wa bao kwa kuvua jezi yake namba 10 mgongoni baada ya kuitandika bao la pili klabu ya Kagera Sugar katika mchezo uliofanyika Jumamosi katika uwanja wa Kaitaba Kagera.
Kutokana na kitendo hicho cha Ajib kuvua jezi yake Mo Dewji anawasanifu wapinzani wake wa jadi Yanga kwa kuwaambia hawataweza kufunga goli zuri kama alilofunga Mshambuliaji wao wa kimataifa raia wa Uganda, Emmanuel Okwi na kusema kama ingetokea wangefunga goli kali kama hilo anaamini kuwa mchezaji wao huyo huenda angevua bukta kabisa.Klabu ya Simba ya Yanga zinategemea kukutana tena Oktoba 28, 2017 ambapo timu zote mbili zimeanza maandalizi kuelekea mchezo huo ambao huwa unavuta hisia kubwa miongoni mwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini Tanzania, na majigambo tayari yameshaanza kama ambavyo tunaona.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...