Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ilikuwa inasemekana yupo kwenye
mahusiano ya kimapenzi na muigizaji wa vichekesho Ebitoke, amemtaka
msanii huyo kuwa na subira juu ya yale anayoona anamkosea na kusema muda
utafka na kila kitu kitakuwa sawa.
Akiongea
kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ben Pol amesema anaamini
mpenzi wake huyo anaelewa mazingira ya kazi zake jinsi yalivyo, na
mchaka mchaka wa ubize ambao alikuwa nao kwenye kazi zake za muziki.
"Mimi naamini anaelewa, saa nyingine uko safarini hakuna
mtandao, nafikiri tuwe na subira vitu vingine vingi tutapata ufumbuzi wa
kila kitu, unajua kila mtu ana mapungufu yake, unaweza ukakosea sehemu
baadaye mkaelewana mkasahau", amesema Ben Pol.Hivi karibuni Ebitoke alisikika akisema kuwa Ben Pol hapokei simu zake wala hajibu message zake, na kuomba watu wamsaidie kumuuliza Ben Pol amekutwa na nini mpaka kufikia hatua hiyo.
No comments:
Post a Comment