
Cristiano Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandanda mwaka huu kwa mara ya pili mfululizo
.
Tuzo hiyo kwa mchezaji bora mwanamke aliinyakuwa mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.
Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliyochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Aliwashinda Lionel Messi wa Barcelona na mchezaji ghali zaidi duniani anayechezea Paris St-Germain, Mbrazil Neymar.
Messi alimpigia kura mwenzake wa Barcelona Luis Suarez naye Ronaldo alimpigia mwenzake wa Real - Luka Modric.
Ronaldo na Messi wakisalimiana |
Ronaldo akiwa na familia yake |
No comments:
Post a Comment