Tuesday, 14 November 2017

tyson azuiwa nchini chile

Mike Tyson akiandamana na maafisa wa polisi wa idara ya uhamiaji katika uwanja wa ndege wa SantiagoBingwa wa uzani mzito duniani Mike Tyson amezuiliwa kuhudhuria sherehe ya kupeana tuzo mjini Santiago, Chile.
Lakini raia huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 51 ambaye aliwahi wakati mmoja kuhudumia kifungo jela kwa ubakaji, unyanyasaji na umiliki wa dawa za kulevya alirudishwa nyumbani na maafisa wa polisi wa idara ya uhamiaji.
Maafisa wa polisi katika uwanja wa Santiago walisema kuwa Tyson alirudishwa nyumbani kwa kufeli kuafikia sheria za uhamiaji.
Tyson alizuiliwa kuingia nchini Uingereza 2013 kutokana na matatizo yaliomkubw wakati wa nyuma.
''Baada ya kutathmini rekodi yake kulingana na sheria za uhamiaji ,wageni wote ambao walihukumiwa kwa kutekeleza uhalifu wowote hawaruhusiwi kuingia nchini humu'', polisi walisema.
Bingwa huyo mara mbili alihudumia miaka mitata jela katika kifungo cha miaka sita 1992 kwa kumbaka mgombea wa shindano la malkia wa urembo nchini humo.
Alikuwa bingwa wa uzani mzito mwenye umri mdogo katika historia ya uzani huo wakati alipomshinda Trevor Berbick 1986.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...