
Kufanya mazoezi kwa dakika 30 kutaboresha mzunguko wa damu
mwilini ambapo kutapelekea kusambazwa kwa hewa ya Oksijeni ( Oxygen) na sukari
(glucose) katika ogani mbali mbali za mwili, hususan katika ubongo. Hii
itatusaidia kuondokana na hali ya uchovu, kupunguza msongo
wa mawazo na kuwa na utulivu.
Katika utafiti mmoja uliochapishwa na jarida la Madawa na
sayansi ya michezo, " Kila tunachofanya hutumia gesi ya Oksijeni , kwa
hiyo kufanya mazoezi huimarisha mifumo ya miili yetu na hutuongezea ufanisi
katika ufanyaji kazi bila kuchoka kwa urahisi, pia huboresha uwezo wa ufanyaji
kazi wa ubongo(kufikiri na kumbukumbu)"
No comments:
Post a Comment