
Mchanganuo mpya umeonyesha kuwa, uwekezaji wa kiasi cha dola
4.70 za kimarekani kwa kila mtoto anayezaliwa, utauingizia uchumi wa dunia takriban
dola 300 bilioni za kimarekani ifikapo mwaka 2025.
GENEVA. Hakuna nchi yeyote duniani iliyoweza kufikia kwa
utimilifu viwango vya unyonyeshaji
watoto ulimwenguni pote, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani WHO na shirika la
watoto UNICEF
wakishirikiana na taasisi ya unyonyeshaji (Global
breastfeeding collective) katika mpango
wa kuongeza viwango ya unyonyeshaji watoto ulimwenguni.
Taasisi hiyo ilifanya upembuzi yakinifu kwa nchi 194 na
kugundua kuwa ni asilimia 40 pekee ya watoto walio chini ya miezi sita
walionyonyeshwa bila kupewa chakula kingine na ni nchi 23 peekee zilizokuwa na
zaidi ya asilimia 60 za viwango vya unyonyeshaji bila kuwapa chakula kingine
watoto walio chini ya umri wa miezi sita.
Utafiti umeonyesha kuwa, unyonyeshaji wa watoto unaboresha afya ya akili, na faida nyingine
nyingi kiafya kwa wote mama na mtoto. Unyonyeshaji wa watoto chini ya miezi
sita bila kuwapa chakula kingine umesaidia
kuwaepusha watoto na magonjwa hatari kama kuhara na homa ya mapafu ambayo ni
magonjwa hatari yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto. Kina mama
wanaonyonyesha wamepunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama saratani ya kizazi
na matiti ambayo ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya kina mama.
"Maziwa ya mama yanampa mtoto mwanzo mzuri wa maisha
yake" Anasema Dr Tedros Adhanom mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani
WHO na anaendelea kusema kuwa, "Maziwa ya mama yanafanya kazi kama chanjo
ya mwanzo kabisa ya mtoto, na huwalinda watoto wachanga dhidi ya magonjwa hatari
pamoja na kuwapatia virutubisho muhimu ambavyo huimarisha afya zao".
Moja ya kisa cha uwekezaji katika unyonyeshaji kwa nchi
zinazoibukia kiuchumi- China, Indonesia, India, Nigeria na Mexico- kushindwa
kuwekeza katika unyonyeshaji kulisababisha vifo vya takriban watoto 236 000 kwa
mwaka pamoja na upotevu wa dola 119 bilioni za kimarekani katika uchumi.
Uwekezaji wa unyonyeshaji ulimwenguni ni wa kiwango cha
chini. Kila mwaka, serikali za nchi za kipato cha chini na cha kati, huwekeza
takriban dola 250 milioni za kimarekani kuhamasisha unyonyeshaji wa watoto na
wafadhili huchangia dola 85 milioni pekee
No comments:
Post a Comment