Sunday, 3 December 2017

MARIO GOTZE NJE HADI 2018 SABABU YA MAJERAHA YA KIFUNDO CHA MGUU

Mario Gotze is one of the greatest players Germany has ever produced, claims Ottmar HitzfieldKiungo wa Borussia Dortmund Mario Gotze atakuwa nja ya dimbani hadi 2018 baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alipata majeraha madogo ya kano la kifundo cha mguu wake wa kulia katika sare ya 4-4 Dortmund dhidi ya Schalke 04.
Gotze amecheza mechi 15 akiwa na BVB msimu huu, akifunga mara moja na kupiga pasi tatu za goli.
Klabu hiyo ya Ujerumani imekuwa kwenye kipindi kigumu na imeshindwa kupata ushidi katika mechi sita za mwisho, na wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakiwa nyuma ya vinara Bayern kwa tofauti ya alama nane.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa wiki sita, ameungana na wengine kwenye orodha ya majeruhi, Marco Reus, Sebastian Rode na Lukasz Piszczek.
Dortmund wataikabili Bayer 04 Leverkusen katika uwanja wa BayArena Jumamosi.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...