Friday, 9 September 2016

msafara wa makamu wa raisi wapata Ajali mkoani Mtwara.

Ni September 9, 2016 ambapo Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara,majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari liliacha njia na nusura kupinduka.
Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
.
.
.
.
.
.
.
.
source: millardAyo

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...