Friday, 9 September 2016

chid benzi kurudi kwenye madawa ya kulevya


Ni Headlines ambazo zimekuwa zikichukua sura tofauti kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva kuhusu taarifa za kwamba  Chid Benz amerudi kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Sasa mengi yamezungumzwa lakini leo Sept 8, 2016 millardayo.com & Ayo TV imempata Kalapina mwanaharakati wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
‘Ni kweli nimepokea taarifa kwamba Chid Benz amerudia kwenye Madawa najaribu kumtafuta sana ili niweze kumrudisha tena Sober House ninaamini tumpe nafasi ya pili kwani dawa za kulevya ni hatari na hii itakuwa mara ya mwisho kwake’
‘Kwa kesi ya Chid Benz mara ya kwanza alisema amepona baada ya kumpeleka kule Sober House lakini tutampeleka tena na kuhakikisha anapata matibabu bora sana na kuachana na Dawa za kulevya’
kalapina

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...