Thursday, 24 September 2015

barcelona apata kipigo dhidi ya celta virgo

Former Liverpool strikerĀ Iago Aspas celebrates scoring the first of his two goals against Barcelona with team-mate Nolito

mchezaji wa zamani wa Liverpool mshambuliaji Iago Aspas akishangilia goli lake alipoifungu barcelona akiwa na mwenzake Nolito
Aspas scored his second before running to the advertising hoardings to celebrate in front of the delighted Celta Vigo fans
hapa mchezaji huyo akishangilia goli lake la pili
Nolito, pictured being mobbed by his team-mates after scoring Celta Vigo's first, also got two assists against his old club in the victory
Barcelona walipokezwa kichapo chao kikubwa zaidi La Liga wakiwa chini ya Luis Enrique baada ya kulazwa 4-1 na Celta Vigo Jumatano.
Kushindwa huko kulifikisha kikomo mapema rekodi yao ya kushinda mechi zao zote msimu huu.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas alifunga mawili baada ya Nolito kuanza ufungaji mabao dhidi ya klabu hiyo yake ya zamani.
Neymar alikomboa moja upande wa Barca zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kuisha, kabla ya nyota wa zamani wa Manchester City na Stoke John Guidetti kufungia wenyeji bao la nne.
Barcelona walikuwa wamepoteza mechi moja pekee kati ya 25 walizocheza majuzi zaidi La Liga.
Ushindi wa Celta uliwaweka kileleni mwa ligi kwa muda, lakini Real Madrid waliwabandua baadaye baada ya kulaza Athletic Bilbao.
Mkufunzi mkuu wa Barca Luis Enrique, alisema: "Kilichoamua mechi hii ni jinsi Celta walivyocheza. Walicheza vyema sana.
“Tulijaribu kuwatatiza lakini walituzidi ujanja. Timu inapokuwa bora kukushinda, huwa huna mengi ya kusema.
"Heri nishindwe na timu inayocheza kama Celta walivyocheza leo, bila kutumia hila, kushinda kwa kucheza vyema soka. Nawapongeza na natumai waendelee kucheza vivyo hivyo.”
Hiyo ilikuwa mara ya tatu kwa Barca kufungwa magoli manne katika mechi tisa walizocheza msimu huu.
Walilazwa 4-0 na Athletic Bilbao katika Super Cup ya Uhispania na pia walicharaza Sevilla 5-4 katika Super Cup ya Uefa.
Neymar pulled one back for Barcelona to make it 3-1, putting it away from close range after a diagonal pass from Lionel Messi
neymar akicheza mpira dhidi ya beki wa celta vigo

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...