Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amemkosoa tena mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger akimtaja kuwa mfalme anayeongoza bila presha
Wenger alidhani kwamba uchokozi wa Diego Costa ndio uliosababisha Gabriel Paulista kupewa kadi nyekundu katika mechi kati ya timu hizo mbili iliochezwa wikiendi iliopita.
Mourinho bila kumtaja mtu yeyote alisema:''Anaweza kuzungumza kuhusu marefa,kuwasukuma watu,unaweza kulia kuanzia asaubuhi hadi jioni lakini hakuna chochote kitakachofanyika.Hawezi kutoa matokeo mazuri lakini bado anaendelea kuwa mfalme''.
Wawili hao wamekuwa na uadui mkubwa huku Mourinho akimwita Wenger kuwa maalum bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment