Saturday, 26 September 2015

simba yalala uwanja wa taifa leo kwa goli 2 kwa nunge(0)

Mfungaji wa goli la kwanza Amis Tambwe (kushoto) akishangilia na Donald Ngoma baada ya kuifungia Yanga goli la kwanza
Mfungaji wa goli la kwanza Amis Tambwe (kushoto) akishangilia na Donald Ngoma baada ya kuifungia Yanga goli la kwanza
Baada ya kusota kwa miaka kadhaa hatimaye leo Yanga wamewatuliza watani zao wa Msimbazi Simba kwa kuwabanjua kwa goli 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara wa raundi ya nne ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Amis Tambwe na Malimi Busungu wameibuka mashujaa kwenye mchezo wa leo lakini sifa pekee zinaenda kwa Busungu aliyeingia kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Msuva na kutengeneza bao lililofungwa na Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza kabla ya yeye kufunga bao la pili dakika ya 79 kipindi cha pili.
Amis Tambwe (kulia) akipongezwa na mshambuliaji mwenzake wa timu hiyo Donald Ngoma
Amis Tambwe (kulia) akipongezwa na mshambuliaji mwenzake wa timu hiyo Donald Ngoma
Simba watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kufunga mabao kipindi cha kwanza wakati wanatawala mchezo kabla ya mambo hayajawa magumu baadae walipofungwa.
Mpira ulianza kwa kasi huku Simba wakitawala sana sehemu kubwa ya mchezo na mara nyingi walitengeneza mashambulizi lakini safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na Hamis Kiiza pamoja Mussa Mgosi ilishindwa kutumia nafasi hizo kufunga magoli.
Muda mwingi wa kipindi cha kwanza Yanga walikuwa wakishambuliwa huku Simba wakitengeneza mashambulizi yao kupitia upande wa winga ya kulia na kumpa Haji Mwinyi kazi ya ziada.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia goli lao la kwanza lililofungwa na Amis Tambwe
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia goli lao la kwanza lililofungwa na Amis Tambwe
Baada ya kuonekana mchezo umemkataa Simon Msuva, kocha wa Yanga alifanya mabadiliko ndani ya kipindi cha kwanza kwa kumtoa Msuva na nafasi yake ikachukuliwa na Malimi Busungu ambaye alionesha uhai mkubwa na badae kutoa pasi ya goli lililofungwa na Amis Tambwe.
Kipindi cha pili mambo yaligeuka baada ya Yanga kumiliki mchezo na kufanya mashabulizi kadhaa kwenye lango la Simba yaliyokuwa na madhara. 
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa hawaamini kilichotokea baada ya timu yao kupigwa bao 2-0 mbele ya Yanga
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa hawaamini kilichotokea baada ya timu yao kupigwa bao 2-0 mbele ya Yanga
Wakati Simba wakipambana kusawazisha goli walilofungwa kipindi cha kwanza, Malimi Busungu alitupia goli la pili na kuzima kabisa matumaini ya kuambulia hata sare kwenye mchezo wa leo. 

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...