Saturday, 26 September 2015

Saudia yakana uvumi wa vifo vya mahujaji

saudi arabia yakana kufa mahujaji zaidi ya 700
Image captionMahujaji waliofariki
Saudi Arabia imekana ripoti kuwa mkanyagano uliowaua zaidi ya watu 700 karibu na mji wa Mecca ulisababishwa na kufungwa kwa barabara ili kuruhusu watu mashuhuri kuingia eneo hilo.
Wizara ya masuala ya ndani ilisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba uvumi huo ulianzishwa na vyombo vya serikali Iran ambayo ilipoteza raia 131.
Iran imeilaumu Saudi Arabia kwa mkasa na ikataka wahusika wote kuchukuliwa hatua za kisheria.
source:bbc swahili 

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...