Thursday, 24 September 2015

Waumini wa dini ya kislamu Morogoro wakataza kampeni msikitini

Waumini wa dini ya kislamu Morogoro wamesema misikiti sio sehemu ya kampeni.
Katika kuadhimisha sikukuu ya Iddi el haji mkoa wa Morogoro viongozi wa dini ya kislamu wamesema misikiti sio mahala pa kampeni za kisiasa na hawapo tayari kuona nyumba za ibada zinatumika kama madaraja ya kuwavusha wanasiasa.
Wakihotubia waumini wa dini ya kislamu kwenye ibada ya sala ya Iddi el haji mkoa wa Morogoro viogozi hao wamewata waumini kushekea sikukuu ya Iddi el haji kwa kuzingatia misingi ya dini yao ambapo pia wa kuendelea kuliombea taifa hasa wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu ili uchaguzi ufanyike kwa haki na amani.
 
Naye mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Rajabu Rutengwe amewataka wananchi kushiriki katika zoezi la uchaguzi kwa amani na utulivu ikiwa ni kutekeleza haki yao ya kideokrasia ya kuchagua viongozi watakao leta mabadiliko ya kweli kwa wananchi.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...