Friday, 25 September 2015

Waziri celina kombani afariki dunia

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya
Utumishi wa Umma nchini Tanzania Celina
Kombani amefariki dunia.
Waziri Kombani ambaye pia alikuwa ni mbunge
wa jimbo la Ulanga mashariki, amefariki jana
Septemba 24, wakati akipata matibabu nchini
India.
Alizaliwa Juni 19, 1959, na alikuwa mbunge
kupitia chama tawala CCM.
Majonzi makubwa lufuatia taarifa za msiba
amefariki dunia leo huko India alikokuwa
akipata matibabu ya saratani.
Tayari mamlaka husika ikiwemo Serikali na
Bunge kupitia ofisi za Bunge zimethibitisha
kifo hicho na kubainisha kuwa, mwili wa
marehemu unategemewa kuwasili Tanzania,
siku ya Jumatatu, na shughuli zote Bunge na
Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko
na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa
marehemu huko Mahenge.
Kabla ya kupatwa na umauti, marehemu alikuwa
Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki na pia
alikuwa akigombea ubunge katika jimbo hilo
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...