Kauli ya Juma Volter Mwapachu Kuhusu Lowassa
Nimekuwa kimya kwa muda mrefu katika mabadilishano ya fikra kwenye mtandao huu ambao kwa hakika, kwa maoni yangu, haubidi kuwa ni wa fikra pevu zisizo shawishika na misimamo ya 'kimalaya ya siasa'.
Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili.
Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili.
Naomba niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo wasomi, wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza na kuhesabika tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa Tanzania. Tuwe wakweli na siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha 'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa maomi na fikra kama vile sisi si wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu kuhusu uongozi wa nchi yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na maana muhimu ya uongozi wa Taifa.
Sasa, Mimi binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa. Yako mengi ambayo kazuliwa huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimu Julius Nyerere alipotamka kwamba 'huyu kijana ninalo faili lake, ana utajiri usiyoelezeka. Ana nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri. Kama Edward alikuwa 'corrupt' swali ni kwanini Baba wa Taifa hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria? Kwanini aseme hayo aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa akiongoza kupendwa dani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa kuwa mgombea wa Urais? Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na hali halisi ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995. Na Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa atoswe kinamna!
Mimi namfahamu Edward, Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa michango hapa na pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya Edward. Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995. Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995. Hivi leo tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo yetu?
Kuhusu hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe, Serikali ilitoa majibu. Mbona kwenye tuhuma za Bunge kuhusu Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo? Nani aliyejaribu kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au kumkomboa kwa kitendo chake cha kujiuzuru kisiasa? Badala yake, wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo facts za kutosha tunaendelea kumshutumu Lowassa na kumwona kama vile ni corrupt na kiongozi asiyefaa. It is not fair.
Mimi simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo kuhusu maamuzi yake. Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu Urais? Jamani, wanazuoni, hivi kweli tumefikia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais? Ili awe au afanye nini ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona, bali pia kuto chukua hatua? Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!!
Taifa letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia kwamba yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusali ghafla yameibuka. Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kubwa na muono mpya.
Juma Volter Mwapachu
No comments:
Post a Comment