Wednesday, 14 October 2015
hakuna urafiki kati ya mwanaume na mwanamke bali kimapenzi
Kati ya vitu vinavyowachanganya watu wengi ni swali kwamba: Je, mwanaume na mwanamke wanaweza kubaki kuwa marafiki na wasijiingize katika uhusiano wa kimapenzi?
Majibu utakayoyapata kutoka kwa watu mbalimbali ni tofauti, lakini yenye mlengo mmoja.
Wengi wanasema kuna urafiki baina ya mwanamke na mwanaume, lakini kwa muonekano huo wa nje huyo rafiki yako alikupenda kimapenzi, lakini akaona akikwambia mapema utamtusi au utamdharau ndiyo maana akaanza kwa staili ya urafiki tu.
Hamna urafiki wa kawaida kati ya mwanaume na mwanamke. Urafiki wa kawaida wa muda mrefu, inasababisha kufikia katika matamanio na kupunguza uelewa wa urafiki wa kuwaida. Wasichana msijiachie kirahisi. Hamna haja ya kuwa na rafiki wa kiume, awe mwanachuo mwenzako, mlio soma naye au rafiki wa kanisani ambaye kwa namna moja au nyingine, kama siyo sasa siku chache zijazo anaweza kuwa mpenzi usiyemtarajia.
Labda ishindikane, pengine kijana awe ni mwenye maadili yaliyokomaa.
Katika uhusiano, mara nyingi huanza kwa msichana kuachia ulinzi wake taratibu. Kijana ataanza kukushika, kukuletea vijizawadi, kukukumbatia na kuku pangusa pangusa nyuma mgongoni na kadhalika. Lazima siku moja utamchekea.
Watu maarufu
Historia inaonyesha kwamba, watu maarufu ndiyo wanaoongoza kwa kuwa katika uhusiano tatanishi wa kuwa na urafiki au kuwa na wapenzi waliowazidi umri.
Mastaa wengi duniani wamekuwa wakishindwa kuaminika, hasa pale wanapojitokeza hadharani na kudai kuwa walio nao ni marafiki wa kawaida. Wengi hushindwa kusadiki hasa kutokana na kujua madhara ya urafiki baina ya mwanamke na mwanaume.
Hata hivyo, wataalamu wa saikolojia wamewahi kusema; hakuna urafiki baina ya mwanamke na mwanaume utakaokwenda sawa, ilmradi mmoja kati yao akaiweka akili yake sawa pasipo kuishughulisha na hisia, jambo ambapo ni nadra kutokea.
“Marafiki wengi waliingia katika uhusiano wa kimapenzi baadaye, kwani uhusiano wa urafiki mara nyingi huzalisha penzi motomoto kwani wawili hawa hupata wasaa mzuri wa kusomana tabia awali,” anasema Blandina Kyando mwanasaikolojia jijini Mbeya.
Wasemavyo wataalamu
Mwanasaikolojia Frank Edward anasema wengi huwa na mawazo kwamba, anapokubali kuwa na rafiki wa jinsia nyingine, anaamini watabaki kuwa marafiki jambo ambalo ni nadra.
Anasema pia kwa wale wanaokuwa na watu waliowazidi umri, huhisi kwamba hao watakuwa msaada kwao kwa kuwashauri mambo makubwa ukilinganisha na wale ambao wana umri sawa, ambao muda mwingi mawazo yao huegemea katika wivu na mengineyo.
“Wanaotafuta wapenzi au marafiki wenye umri mkubwa huhisi watapelekwa katika njia sahihi, na mara nyingi mtu anaweza kuwa na rafiki anayehisi kwamba atakuwa msaada kwake, lakini linapokuja suala la jinsia ni nadra watu hawa kutoingia katika uhusiano wa kimapenzi,” anasema Frank na kuongeza:
“Awali wengi huingia huko kwa nia ya kile wanachokifauata, lakini wanapoendelea kuishi wawili kwa muda fulani, hujikuta wakiondoa wazo la awali na baadaye kuingia katika uhusiano wa kimapenzi.”
Anasema hali huwa ngumu kwa wale walioachwa au kutalikiana. “Unakuta mtu anakwenda kwa mwingine kutafuta faraja, wengine wameachwa na waume au wake zao, hivyo anapokuja mtu hukubali kuwa naye ili kuondoa msongo wa mawazo. Hapa sasa asipoishughulisha akili yake hujikuta akiingia kuwa na uhusiano na mtu asiyefaa au rafiki yake wa karibu,” anasema Frank.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured Post
Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah
Mchezaji wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...
-
Wakati umemualika mwanamke sehemu unayoishi ama wakati umetoka deti katika bar, unapaswa kujua ya kuwa kumsisimua mwanamke huanza kabla ya...
-
Na Baraka Mbolembole Wawakili waTanzania Bara katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, timu ya Yanga SC Jumamosi hii watakuwa na kib...
-
Mao alikuwa kiongozi Kichina Kikomunisti na mwanzilishi wa Jamhuri ya Watu wa China. Yeye alikuwa kuwajibika kwa sera za maafa ya ...
No comments:
Post a Comment