Kampuni ya microsoft imezindua laptopu inayojulikana kama surface book ikiwa miongoni mwa bidhaa mpya za Windows 10.
Microsoft pia imetoa simu mbili aina ya smartphone,ikiwa ni toleo jipya la tablets.
Mengi yanatarijiwa katika uzinduzi huo huku mkuu wa kampuni hiyo Satya Nadella akitaka kuthibitisha kwamba kampuni hiyo inaweza kutoa ushindani mkubwa kwa wapinzani wake.
Wachanganuzi wanasema kuwa laptopu hiyo huenda ikasaidia kuimarisha soko la kompyuta za kibinafsi.
Laptopu hiyo ikiwa ni ya kwanza kuzinduliwa na kampuni ya Microsoft ilikuwa miongoni mwa bidhaa za Microsoft zilizozinduliwa katika hafla mjini New York.
Imetengezwa kushindana na Apple Macbook,huku microsoft ikilinganisha bidhaa hizo moja kwa moja.
source:http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151006_kompyuta-mac-book
No comments:
Post a Comment