Wednesday, 7 October 2015

jurgen klopp akaribia kusaini liverpool baada ya brendan rodgers

MJERUMANI Jurgen Klopp anatarajiwa ikutambulishwa Ijumaa kuwa kocha mpya wa Liverpool, kufuatia kufukuzwa kwa Brendan Rodgers. 
Mazungumzo yamekuwa yakifanyika na washauri wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 tangu Jumapili na Liverpool wanajiamini mno kwamba watampata kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund
Mkataba bado haujasainiwa, lakini inatarajiwa kwamba Klopp atapewa isiyopungua miaka mitatu na kampuni ya Fenway Sports Group, wamiliki wa Liverpool kama ambavyo walifanya kwa watangulizi wake, Kenny Dalglish na Brendan Rodgers.  
Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Jugern Klopp amekuwa kwenye rada za Fenway Sports Group, wamiliki wa Liverpool arithi mikoba ya Rodgers

Klopp amekuwa kwenye rada za FSG ili achukua nafasi ya Rodgers a mipango imekuwa ikipelekwa haraka haraka kuhakikisha hawapotezi fursa ya kumpata kocha huyo mwenye hadhi ya juu katika mchezo huo Ulaya. 
Anatarajiwa kuwachukua Wasaidizi wake wa muda mrefu, Zelkjo Buvac na Peter Krawietz akafanye nao kazi, ingawa bado mustakabali wa Sean O'Driscoll, Gary McAllister na Pepijn Lijnders, ambao wote waliteuliwa na Rodgers haujajulikana. 
reus akifanya yake kwenye klabu ya dortumund chini ya kocha klopp, reus anapiga kwenda kwa lewandowisk 

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...