Wednesday, 14 October 2015

Uchumi supermarket yafungwa nchi Tanzania

Image captionUchumi
Wafanyikazi na wasambazaji wa bidhaa waliojawa na hasira kutoka kwa duka la jumla la Uchumi Supermarket wamelazimisha kufungwa kwa mojawapo ya maduka hayo nchini Tanzania.
Zaidi ya wafanyikazi 300 walizuia kufunguliwa kwa duka hilo kwa hofu kwamba hawatalipwa fedha zao.
Kumekuwa na ripoti kwamba maduka hayo ambayo yalinzishwa nchini Kenya huenda yakafunga baadhi ya biashara zake.
Matatizo ya kifedha yamelazimu Uchumi kufunga baadhi ya maduka yake nchini Uganda.
Hatahivyo Uchumi imesema kuwa mazungumzo yanaendelea kutatua mzozo huo.
Mwandishi wa BBC Alice Muthengi mjini Daresalam anasema kuwa wafanyikazi hao waliagizwa kurudi nyumbani na kurudi siku ya jumatano ,ambapo suluhu itapatikana.
Uchumi ina maduka maduka kadhaa nchini Tanzania lakini haijulikani ni mangapi yataathiriwa.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...