Tuesday, 17 November 2015

Lulindi wasusia uchaguzi

Wananchi wa Lulindi wasusia uchaguzi baada ya kutoridhishwa na uchaguzi uliyomalizika Octobar 25.
Wananchi wa jimbo la Lulindi wengi wakiwa vijana wamesusia uchaguzi wa mbunge baada ya kutoridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu uliyomalizika Octobar 25 mwaka huu kwa madai mfumo wa siasa bado umeegemea chama kimoja na si vyama vingi.
ITV imetembelea baadhi ya vituo katika kata za Chiungtwa, Namalenga, na Lulindi na kukuta sehemu kubwa ya vituo havina watu lakini pia iliweza kupita muda wa dakika tatu mpaka tano anajitokeza mpiga kura mmojammoja kama anavyozungumza msimamizi Romanus Charles.
 
Wengi waliojitokeza katika uchaguzi huo ni wazee wenye umri mkubwa na wakina mama wenye umri wakati, hata hivyo wagombea pia walijitokeza kupiga kura na wakawa na ujumbe huu.
 
Jimbo la Lulindi linawapiga kura elfu 59 miasita 19 huku likiwa na vituo vya kupigia kura 199, kata kumi na nane, limelazimika kurudia uchaguzi baada ya jina la mgombea ubunge wa CUF kukosewa.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...