Tuesday, 17 November 2015

spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania ndugu Ndugai

Mh.Ndugai ashinda kiti cha uspika wa bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza mkutano wake mkoani Dodoma huku mbunge wa Kongwa Job Ndugai wa chama cha mapinduzi akishinda kiti cha spika wa bunge hilo dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha demokrasia na maendeleo–Chadema Dr. Godluck Ole Medeye na madhaifu ya ukumbi huo wa kisasa wa bunge yakijionyesha ikiwemo baadhi  ya vipaza sauti kushindwa kufanya kazi.
Akitangaza matokeo ya kiti hicho cha uspika, mwenyekiti wa muda wa wabunge hao Andrew Chenge amesema Mhe. Ndugai ameshinda kiti hicho baada ya kwa kupata kura 254 na kumshinda  mpinzani wake mkuu  Dr. Godluck Ole Medeye wa chama cha demokrasia na maendeleo –Chadema aliyepata kura 109 na wagombea wengine sita waliosalia wakishindwa kupata kura hata moja.
 
Na kisha spika huyo mteule akaapa na kuwa spika kamili Naye Mhe.Ndugai amesema atahakikisha anatumikia kiti hicho cha uspika kwa uadilifu mkubwa huku aliyekuwa mpinzani wake mkuu Dr.Godluck Ole Medeye akisema kuwa huo ni mwanzo na atahakikisha anakuwa kinara wa kuendeleza demokrasia hapa nchini.
 
Baada ya hapo vikafuata viapo vya baadhi ya waheshimiwa wabunge.
 
Awali bungeni hapo ilijitokeza dosari kwa vifaa vya kupaza sauti kushindwa kufanya kazi hali iliyosababisha baadhi ya shughuli bungeni hapo kusimama mara kwa mara.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...